Machapisho

MWELEKEO WA MVUA ZA MASIKA (MAM) 2025 KWA MKOA WA MARA

Pakua

(i)Kwa ujumla mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo ya magharibi mwa mkoa wa Mara na Wastani hadi Juu ya Wastani katika maeneo ya mashariki mwa mkoa.

(ii)Mvua zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Machi, 2025.

(iii)Mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya kwanza ya mwezi Mei, 2025.

(iv)Upo uwezekano wa kutokea vipindi vya ukavu vya siku kumi (10) au zaidi katika msimu huu wa Masika, 2025.