Machapisho

Mkataba wa Huduma Kwa Mteja

Pakua

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Na.2 ya mwaka 2019 kupitia Tangazo la Serikali GN.459 la tarehe 14 Juni 2019. Taasisi hii ni ya Muungano na ina majukumu ya kutoa huduma za hali ya hewa, kudhibiti, pamoja na kuratibu shughuli za hali ya hewa nchini. Aidha, Mamlaka ina jukumu la kuiwakilisha nchi katika masuala ya hali ya hewa kimataifa.