Machapisho

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI JANUARI, 2025

Pakua

Dondoo za tathmini ya Desemba, 2024 na mwelekeo wa Januari, 2025:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Desemba, 2024 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Januari, 2025 nchini.

  • Katika kipindi cha mwezi Desemba, 2024 baadhi ya maeneo nchini yalipata mvua za wastani. Aidha, vipindi vya mvua kubwa vilijitokeza katika baadhi ya maeneo na kusababisha athari ikiwemo mafuriko na kutuama kwa maji.
  • Katika kipindi cha mwezi Januari 2025, mvua zinatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka ikiashiria muendelezo wa mvua za Msimu. Hata hivyo, mvua za nje ya msimu zinatarajiwa katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Aidha, ongezeko la mvua linatarajiwa katika baadhi ya maeneo.