Machapisho

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI DISEMBA, 2024

Pakua

Dondoo za tathmini ya Novemba, 2024 na mwelekeo wa Disemba, 2024:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Novemba, 2024 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Disemba, 2024 nchini.

  • Katika kipindi cha mwezi Novemba, 2024 vipindi vya mvua viliendelea kujitokeza katika baadhi ya maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka vipindi vya mvua vilijitokeza ikiashiria kuanza kwa mvua za Msimu, 2024/2025. Aidha, ongezeko la mvua lilijitokeza katika baadhi ya maeneo hususan katika wiki ya tatu na ya nne.
  • Hali ya joto iliendelea kujitokeza katika baadhi ya maeneo nchini, hususan maeneo ya ukanda wa pwani na nyanda za juu kaskazini mashariki katika kipindi cha Novemba 2024.
  • Katika kipindi cha mwezi Disemba 2024, mvuazinatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi nchini. Aidha, ongezeko la mvua linatarajiwa katika baadhi ya maeneo.