Machapisho

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI NOVEMBA, 2024

Pakua

Dondoo za tathmini ya Oktoba, 2024 na mwelekeo wa Novemba, 2024:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Oktoba, 2024 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Novemba, 2024 nchini.

  • Katika kipindi cha mwezi Oktoba, 2024 vipindi vya mvua vilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini, hususan yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka ikiashiria kuanza kwa mvua za Vuli, 2024. Aidha, vipindi vichache vya mvua kubwa vilijitokeza.
  • Katika kipindi cha mwezi Novemba 2024, mvua za Msimu zinatarajiwa kuanza katika maeneo mengi yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. Aidha, mvua za Vuli zinatarajiwa kuendelea huku kikiwa na uwezekano wa ongezeko la mvua katika baadhi ya maeneo.
  • Hali ya joto inatarajiwa kuendelea katika maeneo yanayotarajiwa kuwa na upungufu wa mvua.