Machapisho

MWELEKEO WA MVUA ZA MSIMU (NOVEMBA, 2024 – APRILI, 2025) KWA MKOA WA MBEYA

Pakua

(i)Kwa ujumla mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya kusini, na wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Mbeya.

(ii)Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Novemba, 2024.

(iii)Mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya kwanza ya mwezi Mei, 2025.

(iv)Upungufu wa mvua unatarajiwa katika nusu ya kwanza ya msimu (Novemba, 2024 - Januari, 2025).