Machapisho
MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA ZA VULI (OKTOBA– DISEMBA), 2024 KWA MAENEO YA KASKAZINI MWA MKOA WA MOROGORO
Pakua(i).Kwa ujumla mvua za Chini ya Wastani hadi Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro.
(ii).Mvua zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Oktoba, 2024.
(iii).Mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya nne ya mwezi Disemba, 2024.
(iv).Vipindi virefu vya ukavu vya siku kumi (10) au zaidi vinatarajiwa katika msimu huu wa Vuli.