Machapisho
MWELEKEO WA HALI YA HEWA WA MWEZI AGOSTI, 2024
PakuaDondoo za tathmini ya Julai, 2024 na mwelekeo wa Agosti, 2024:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Julai, 2024 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto kwa mwezi Agosti, 2024 nchini.
i. Katika kipindi cha mwezi Julai, 2024 vipindi vya baridi hadi baridi kali viliendelea kujitokeza katika baadhi ya maeneo nchini hususani nyakati za usiku na asubuhi.
ii. Vipindi vya upepo mkali vilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini, hususan ukanda wa Pwani na maziwa makuu katika kipindi cha mwezi Julai, 2024. Kwa upande mwingine, vipindi vichache vya mvua vilijitokeza katika ukanda wa ziwa Victoria, ukanda wa pwani na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki.
iii. Katika kipindi cha mwezi Agosti 2024, hali ya ukavu inatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi nchini pamoja na hali ya baridi hadi baridi kali katika baadhi ya maeneo. Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache ya mwambao wa pwani na ukanda wa Ziwa Victoria na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki. Aidha, vipindi vya upepo mkali vinatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo nchini.