Machapisho
TAARIFA YA HALI MBAYA YA HEWA KWA MWEZI MEI NA JUNI, 2024
PakuaKatika kipindi cha mwezi ya Mei, 2024 vipindi vya mvua viliendelea kujitokeza katika baadhi ya maeneo ya nchi, hususan katika nusu ya kwanza ya mwezi. Aidha, kutokea kwa kimbunga Hidaya kulisababisha vipindi vya mvua kubwa katika maeneo ya pwani ikiwemo mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani na kupelekea mafuriko na uharibifu wa mali na miundombinu. Katika kipindi cha mwezi Juni, 2024 vipindi vya upepo mkali na baridi vilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini ikiashiria kuanza kwa msimu wa Kipupwe, 2024.