Machapisho
MWELEKEO WA HALI YA HEWA JULAI 2024
PakuaDondoo
za tathmini ya Juni, 2024 na mwelekeo wa Julai, 2024:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Juni, 2024 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto kwa mwezi Julai, 2024 nchini.
i.Katika kipindi cha mwezi Juni, 2024 vipindi vya baridi vilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini hususani nyakati za usiku na asubuhi.
ii.Kwa mwezi Juni, 2024 vipindi vifupi vya upepo mkali vilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini, husasan ukanda wa Pwani na maziwa makuu. Kwa upande mwingine, vipindi vichache vya mvua vilijitokeza katika ukanda wa ziwa Victoria, ukanda wa pwani na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki.
iii.Katika kipindi cha mwezi Julai 2024, hali ya ukavu na baridi inatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi nchini. Aidha, vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache ya mwambao wa pwani na ukanda wa Ziwa Victoria. Pia,vipindi vya upepo mkali vinatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo nchini.