Machapisho

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI OKTOBA, 2021

Pakua

Dondoo za tathmini ya Septemba, 2021 na mwelekeo wa Oktoba, 2021:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Septemba, 2021 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Oktoba, 2021 nchini.

  • Katika kipindi cha mwezi Septemba, hali ya baridi ya kawaida iliripotiwa katika baadhi ya maeneo nchini. Kiwango cha chini zaidi cha joto kiliripotiwa katika maeneo ya nyanda za juu kusini magharibi, kanda ya kusini na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki. Kwa upande mwingine, vipindi vya upepo mkali unaofikia km 40 kwa saa viliripotiwa katika maeneo ya pwani.
  • Katika mwezi Oktoba, 2021 mvua za Vuli zinatarajiwa kuanza katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Aidha, maeneo machache ya Ukanda wa ziwa Victoria na pwani yanatarajiwa kuendelea kupata vipindi vya mvua. Viwango vya joto vinatarajiwa kuongezeka katika baadhi ya maeneo nchini.

Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua;