Machapisho

MWELEKEO WA HALI YA HEWA WA MWEZI MEI, 2024

Pakua

Dondoo za tathmini ya Aprili, 2024 na mwelekeo wa Mei, 2024:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Aprili, 2024 pamoja na mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Mei, 2024 nchini.

  • Katika kipindi cha mwezi Aprili, 2024 vipindi vya mvua vilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini mengi pamoja na vipindi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo na kusababisha mafuriko, uharibifu wa mali, miundombinu na upotevu wa maisha.
  • Katika kipindi cha mwezi Mei 2024, mvua zinatarajiwa kuendelea katika baadhi ya maeneo hususan yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Aidha, ongezeko la mvua linatarajiwa katika maeneo machache.
  • Joto la kawaida hadi juu kidogo ya kawaida linatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi kwa kipindi cha mwezi Mei, 2024.