Machapisho

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI APRILI, 2024

Pakua

Dondoo za tathmini ya Machi, 2024 na mwelekeo wa Aprili, 2024:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Machi, 2024 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Aprili, 2024 nchini.
i. Katika kipindi cha mwezi Machi, 2024 vipindi vya mvua vilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini pamoja na vipindi vya mvua kubwa katika maeneo machache na kusababisha mafuriko na uharibifu wa mali na miundombinu.
ii. Katika kipindi cha mwezi Aprili 2024, mvua zinatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi. Aidha, vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo.
iii. Joto la kawaida hadi juu kidogo ya kawaida linatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi kwa kipindi cha mwezi Aprili, 2024.