Machapisho
MATARAJIO YA HALI YA HEWA KWA TAREHE 01 - 10 NOVEMBA, 2024
PakuaMWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 01-10 NOVEMBA, 2024
Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Mvua na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.
Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaampamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Mvua zinatarajiwa katika maeneo machache.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Mvua na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.
Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Mvua na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Mvua zinatarajiwa katika maeneo machache.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro: Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.
Imetolewa na;
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA