Machapisho

MATARAJIO YA HALI YA HEWA KWA TAREHE 21 - 31 MEI, 2021

Pakua

MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 21- 31 MEI, 2021.

Kanda ya ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Vipindi vya mvua na ngurumo za radi katika maeneo machache hususan katika nusu ya kwanza ya dekadi.

Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro,): Mvua nyepesi katika maeneo machache.

Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Mvua nyepesi katika maeneo machache.

Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Vipindi vya ngurumo za radi, vikiambatana na vipindi vifupi vya mvua katika maeneo machache.

Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla.

Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla.

Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla.

Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla.

Imetolewana; MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Kwa taarifa zaidi, tafadhali pakua...