Machapisho
MWELEKEO WA MVUA ZA MASIKA (MACHI-MEI), 2024
PakuaDondoo muhimu za msimu wa mvua za Masika; Machi - Mei 2024
Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua za Masika katika kipindi cha Machi – Mei, 2024, ushauri kwa wadau wa sekta na mamlaka mbalimbali kama vile Kilimo na Usalama wa Chakula, Mifugo na Uvuvi, Utalii na Wanyamapori, Uchukuzi, Mamlaka za miji, Nishati, Maji na Madini, Afya pamoja na Menejimenti za Maafa. Baadhi ya mambo muhimu katika taarifa hii ni: -
i. Mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani kwa msimu wa Masika, 2024 zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.
ii. Ongezeko la mvua linatarajiwa katika kipindi cha mwezi Machi, 2024.
iii. Mvua za Masika zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Februari, 2024 katika maeneo mengi na zinatarajiwa kuisha katika wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei 2024 katika maeneo mengi.
Athari zinazotarajiwa:
i. Vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na miundombinu ya kilimo.
ii. Kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kuongezeka.
iii. Magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza kutokana na uchafuzi wa maji