Machapisho

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI FEBRUARI, 2024

Pakua

Dondoo za tathmini ya Januari, 2024 na mwelekeo wa Februari, 2024:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Januari, 2024 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Februari, 2024 nchini.

i.Katika kipindi cha mwezi Januari, 2024 maeneo mengi ya nchi yaliendelea kupata mvua za juu ya wastani. Aidha, vipindi vya mvua kubwa vilijitokeza katika baadhi ya maeneo na kusababisha athari ikiwemo mafuriko na uharibifu wa mali na miundombinu.

ii.Katika kipindi cha mwezi Februari 2024, mvua za msimu zinatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. Hata hivyo, mvua za nje ya msimu zinatarajiwa pia katika baadhi ya maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Aidha, ongezeko la mvua linatarajiwa katika baadhi ya maeneo nchini.