Machapisho
TAARIFA YA HALI MBAYA YA HEWA KWA MWEZI DISEMBA 2023
PakuaKatika kipindi cha mwezi Disemba, 2023 vipindi vya mvua vilijitokeza katika maeneo mengi ya nchi. Aidha, maeneo mengi yalipata mvua za wastani hadi juu ya wastani ikilinganishwa na wastani wa muda mrefu wa mwezi Disemba. Vipindi vya mvua kubwa vilijitokeza katika baadhi ya maeneo na kusababisha mafuriko, ongezeko la unyevu ardhini na kina cha maji. Vilevile, vipindi vya upepo mkali vilijitokeza katika maeneo machache ya ukanda wa Pwani na nyanda za juu kaskazini mashariki. Hali ya hewa iliyojitokeza pamoja na athari zake imeendana na taarifa ya mwelekeo wa mvua za Vuli (Oktoba-Disemba), 2023 kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka na mwelekeo wa mvua za Msimu, 2023/2024 kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka.