Machapisho
TAARIFA YA HALI MBAYA YA HEWA KWA MWEZI NOVEMBA 2023
PakuaKatika kipindi cha mwezi Novemba, 2023 vipindi vya mvua vilijitokeza katika maeneo mengi ya nchi. Aidha, maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka yalipata mvua za juu ya wastani ukilinganisha na wastani wa muda mrefu wa mwezi Novemba. Hali hii ilisababisha mafuriko, ongezeko la unyevu ardhini, kina cha maji na malisho kwa baadhi ya maeneo. Hata hivyo, vipindi vya upepo mkali vilijitokeza katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani, kati mwa nchi, nyanda za juu kaskazini mashariki na nyanda za juu kusini magharibi. Hali ya hewa iliyojitokeza pamoja na athari zake imeendana na taarifa ya mwelekeo wa mvua za Vuli (Oktoba-Disemba), 2023 pamoja na mvua za Msimu, 2023/2024.