Machapisho
MWELEKEO WA HALI YA HEWA DISEMBA 2023
PakuaDondoo za tathmini ya Novemba, 2023 na mwelekeo wa Disemba, 2023:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Novemba, 2023 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Disemba, 2023 nchini.
i.Katika kipindi cha mwezi Novemba, 2023 maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka yalipata mvua za juu ya wastani ukilinganisha na wastani wa muda mrefu wa mvua za mwezi Novemba. Aidha, vipindi vya mvua kubwa zilizopelekea kutokea kwa mafuriko vilijitokeza katika baadhi ya maeneo. Kwa upande mwingine, vipindi vya mvua vilijitokeza katika baadhi ya maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka ikiashiria kuanza kwa mvua za Msimu, 2023/2024.
ii.Katika kipindi cha mwezi Disemba 2023, mvua zinatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi ya nchi. Aidha, ongezeko la mvua linatarajiwa katika baadhi ya maeneo.