Machapisho
TAARIFA YA HALI MBAYA YA HEWA KWA MWEZI SEPTEMBA NA OKTOBA 2023
PakuaKatika kipindi cha mwezi Septemba 2023 hali ya ukavu iliendelea kujitokeza katika maeneo mengi ya nchi ikiambatana na hali ya joto. Aidha, kwa mwezi Oktoba, 2023 ongezeko kidogo la mvua lilijitokeza katika baadhi ya maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka ikiashiria kuanza kwa msimu wa mvua za Vuli, 2023. Hali hii ilisababisha ongezeko kidogo la unyevu ardhini, kina cha maji na malisho kwa maeneo machache. Hata hivyo, vipindi vya upepo mkali vilijitokeza katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani, kati mwa nchi, nyanda za juu kusini magharibi na maeneo ya maziwa makuu. Hali ya hewa iliyojitokeza pamoja na athari zake imeendana na taarifa ya mwelekeo wa mvua za Vuli (Oktoba-Disemba), 2023.