Machapisho
MWELEKEO WA MVUA ZA MSIMU (NOVEMBA, 2023 – APRILI, 2024) KWA MAENEO YA KUSINI MWA MKOA WA MOROGORO
Pakua(i)Kwa ujumla mvua za juu ya wastani hadi wastani zinatarajiwa katika maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro.
(ii)Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Novemba, 2023.
(iii)Mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Aprili, 2024.
(iv)Upo uwezekano wa kutokea vipindi vya ukavu vya siku 10 au zaidi hususan katika mwezi Februari, 2024.