Machapisho
TAARIFA YA HALI MBAYA YA HEWA KWA MWEZI JULAI NA AGOSTI, 2023
PakuaKatika kipindi cha mwezi Julai hadi Agosti, 2023 hali ya ukavu, baridi ya wastani hadi baridi kali iliendelea kujitokeza katika maeneo mengi nchini na kusababisha upungufu wa unyevu ardhini, kupungua kwa maji na malisho pamoja na kuwepo kwa hali vumbi. Hata hivyo, vipindi vya upepo mkali pia vilijitokeza na kuathiri maeneo ya ukanda wa pwani, kati mwa nchi, nyanda za juu kusini magharibi na maeneo ya maziwa makuu.
Ingawa hali ya ukavu imeendelea kujitokeza katika maeneo mengi ya nchi lakini matukio machache ya mvua yalijitokeza katika maeneo ya ukanda pwani, ziwa Victoria na nyanda za juu kaskazini mashariki. Aidha, hali ya hewa iliyojitokeza pamoja na athari zake imeendana na taarifa ya mwelekeo wa msimu wa Kipupwe (Juni-Agosti), 2023.