Machapisho
UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI OKTOBA, 2023
PakuaDondoo za tathmini ya Septemba, 2023 na mwelekeo wa Oktoba, 2023:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Septemba, 2023 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Oktoba, 2023 nchini.
i. Katika kipindi cha mwezi Septemba, 2023 hali ya ukavu iliendelea kujitokeza katika maeneo mengi nchini. Hata hivyo, vipindi vichache vya mvua vilijitokeza katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani, nyanda za juu kaskazini mashariki, ukanda wa ziwa Victoria na maeneo ya magharibi mwa nchi. Aidha, vipindi vya baridi vilijitokeza katika maeneo machache hususani nyanda za juu kusini magharibi.
ii. Katika kipindi cha mwezi Oktoba 2023, mvua za Vuli zinatarajiwa kuanza katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Aidha, ongezeko kidogo la joto linatarajiwa katika baadhi ya maeneo nchini.