Machapisho
MWELEKEO WA MVUA ZA VULI (OKTOBA-DISEMBA) 2023 KWA MKOA WA KAGERA
Pakua(i)Msimu huu unatarajiwa kutawaliwa na hali ya El Nino ambayo inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika mwenendo wa mvua za msimu wa Vuli, 2023.
(ii)Kwa ujumla mvua za Juu ya Wastani hadi Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya mkoa wa Kagera.
(iii)Mvua zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya nne ya mwezi Septemba na ya kwanza ya mwezi Oktoba, 2023.
(iv)Mvua zinatarajiwa kuendelea hadi mwezi Januari, 2024.
(v)Upo uwezekano wa kutokea vipindi vya ukavu vya siku kumi (10) au zaidi katika msimu huu wa Vuli.