Machapisho
MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA KIPINDI CHA MSIMU WA VULI (OKTOBA – DISEMBA), 2020
PakuaDondoo muhimu za msimu wa mvua za Vuli kipindi cha Oktoba – Disemba, 2020
Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli kipindi cha Oktoba - Disemba 2020, ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na uvuvi, maliasili, wanyamapori na utalii, nishati na maji, usafirishaji (nchi kavu, kwenye maji na angani), mamlaka za miji, afya pamoja na menejimenti za maafa. Utabiri huu ni mahsusi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka (Nyanda za juu kaskazini mashariki, Pwani ya kaskazini, Ukanda wa Ziwa Viktoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma). Kwa muhtasari, mwelekeo huo na athari zake unaonesha kuwa:
a)Mvua za Vuli, 2020
i. Mvua za Vuli zinatarajiwa kuwa za chini ya wastani hadi wastani na zitakazoambatana na vipindi virefu vya ukavu katika maeneo mengi ya nchi.
ii. Mvua za Vuli zinatarajiwa kuanza kwa kuchelewa kati ya wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Novemba, 2020 katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki, na ukanda wa pwani ya Kaskazini pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Morogoro.
b)Athari zinazotarajiwa
i. Upungufu wa unyevunyevu katika udongo unatarajiwa kujitokeza katika maeneo mengi.
ii. Kujitokeza kwa magonjwa ya mlipuko, kutokana na upungufu wa maji safi na salama.
iii. Upungufu wa malisho na maji unaweza kujitokeza hivyo kusababisha kujitokeza kwa migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
iv. Uwezekano wa kutokea matukio ya moto katika mapori na misitu, hivyo mamlaka husika zinashauriwa kupanga mikakati mahsusi ya kukabiliana na hali hiyo.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali pakua