Machapisho
MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA ZA VULI (OKTOBA – DISEMBA), 2023 KWA MAENEO YA KASKAZINI MWA MKOA WA MOROGORO
Pakua(i)Msimu huu unatarajiwa kutawaliwa na hali ya El Nino ambayo inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika mwenendo wa mvua za msimu wa Vuli, 2023.
(ii)Kwa ujumla mvua za Juu ya Wastani hadi Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro.
(iii)Mvua zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Oktoba, 2023.
(iv)Mvua zinatarajiwa kuisha kati ya wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Januari, 2024.
(v)Upo uwezekano wa kutokea vipindi vya ukavu vya siku kumi (10) au zaidi katika msimu huu wa Vuli.