Machapisho
UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI AGOSTI, 2023
PakuaDondoo za tathmini ya Julai, 2023 na mwelekeo wa Agosti, 2023:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Julai, 2023 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto kwa mwezi Agosti, 2023 nchini.
- Katika kipindi cha mwezi Julai, 2023 vipindi vya baridi vilijitokeza katika maeneo mengi nchini hususani nyakati za usiku na asubuhi. Vipindi vya baridi kali zaidi vilijitokeza katika maeneo ya nyanda za juu kusini magharibi na sehemu za miinuko za nyanda za juu kaskazini mashariki.
- Kwa mwezi Julai, 2023 vipindi vifupi vya upepo mkali vilijitokeza katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani pamoja na maziwa makuu. Aidha, vipindi vichache vya mvua vilijitokeza katika maeneo ya ukanda wa pwani na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki.
- Katika kipindi cha mwezi Agosti 2023, hali ya ukavu na baridi inatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi nchini. Ongezeko kidogo la viwango vya joto la chini linatarajiwa katika baadhi ya maeneo nchini kuelekea mwishoni mwa mwezi. Vipindi vya upepo mkali pia vinatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo nchini. Aidha, vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache ya mwambao wa pwani, ukanda wa Ziwa Victoria na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki.