Machapisho
MWELEKEO WA HALI YA HEWA JULAI 2023
PakuaDondoo za tathmini ya Juni, 2023 na mwelekeo wa Julai, 2023:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Juni, 2023 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto kwa mwezi Julai, 2023 nchini.
i.Katika kipindi cha mwezi Juni, 2023 vipindi vya baridi vilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini hususani nyakati za usiku na asubuhi.
ii.Kwa mwezi Juni, 2023 vipindi vifupi vya upepo mkali vilijitokeza katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani. Kwa upande mwingine, vipindi vichache vya mvua vilijitokeza katika ukanda wa ziwa Victoria, ukanda wa pwani na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki.
iii.Katika kipindi cha mwezi Julai 2023, hali ya ukavu na baridi inatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi nchini. Aidha, vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache ya mwambao wa pwani na ukanda wa Ziwa Victoria. Vipindi vya upepo mkali pia vinatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo nchini.