Machapisho
MATARAJIO YA HALI YA HEWA KWA TAREHE 21 - 31 JANUARI, 2024
PakuaMWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 21-31 JANUARI, 2024
Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa
ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Mvua
na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo
machache.
Nyanda za juu
kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache.
Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vya mvua zitakazoambatana na ngurumo za radi
vinatarajiwa kwa baadhi ya maeneo.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya
Kigoma, Katavi na Tabora): Mvua
na ngurumo za radi vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Vipindi vya mvua zitakazoambatana na ngurumo za radi
vinatarajiwa katika maeneo machache.
Nyanda za juu Kusini-magharibi
(Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Vipindi vya mvua zitakazoambatana na ngurumo za radi
vinatarajiwa katika maeneo mengi.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Mvua na ngurumo vinatarajiwa katika maeneo mengi.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Vipindi vya mvua zitakazoambatana na ngurumo za radi
vinatarajiwa katika maeneo mengi.
Imetolewa na;
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA