Machapisho

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI JUNI, 2023

Pakua

Dondoo za tathmini ya Mei, 2023 na mwelekeo wa Juni, 2023:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Mei, 2023 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto kwa mwezi Juni, 2023 nchini.

  • Katika kipindi cha mwezi Mei, 2023 baadhi ya maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka yalipata vipindi vya mvua sambamba na vipindi vifupi vya mvua kubwa vilivyojitokeza katika maeneo machache.
  • Mwezi Juni 2023, hali ya joto la chini inatarajiwa kupungua katika maeneo mengi ya nchi ikiashiria kuanza kwa msimu wa Kipupwe (Juni-Agosti), 2023. Aidha, vipindi vya mvua vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mwambao wa pwani pamoja na maeneo machache ya ukanda wa Ziwa Victoria.