Machapisho

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI MEI, 2023

Pakua

Dondoo za tathmini ya Aprili, 2023 na mwelekeo wa Mei, 2023:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Aprili, 2023 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Mei, 2023 nchini.

  • Katika kipindi cha mwezi Aprili 2023, maeneo mengi nchini yalipata vipindi vya mvua kutokana na kuendelea kuimarika kwa Ukandamvua. Aidha, vipindi vya mvua kubwa vilijitokeza katika baadhi ya maeneo hususani maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.
  • Katika mwezi Mei 2023, vipindi vya mvua vinatarajiwa kuendelea katika baadhi ya maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Aidha, upungufu wa mvua unatarajiwa katika maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka.
  • Ongezeko kidogo la joto linatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo ya nchi hususani maeneo yanayotarajiwa kuwa na upungufu wa mvua kwa kipindi cha mwezi Mei, 2023.