Machapisho
MATARAJIO YA HALI YA HEWA KWA TAREHE 01 - 10 AGOSTI, 2023
PakuaMWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 01- 10 AGOSTI, 2023
Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla na yenye hali ya ubaridi. Hata hivyo, vipindi vifupi vya mvua nyepesi katika maeneo ya miinuko vinatarajiwa.
Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vifupi vya vya mvua nyepesi yenye upepo wa wastani hadi mkali na mawimbi makubwa baharini vinatarajiwa.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu na yenye hali ya ubaridi.
Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa). Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu na yenye hali ya ubaridi.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu na yenye hali ya ubaridi pamoja na vipindi vifupi vya mvua nyepesi yenye upepo wa wastani hadi mkali na mawimbi makubwa baharini vinatarajiwa.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu na yenye hali ya ubaridi.
Imetolewa na;
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA