Machapisho
MATARAJIO YA HALI YA HEWA KWA TAREHE 21 - 30 APRILI, 2023.
PakuaMWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 11-20 APRILI, 2023.
Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Mvua na ngurumo za radi zinatarajiwa.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Mvua na ngurumo za radi zinatarajiwa.
Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Mvua zinazoambata na ngurumo za radi zinatarajiwa kwa baadhi ya maeneo.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Mvua na ngurumo za radi zinatarajiwa.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa.
Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Mvua na ngurumo za radi zinatarajiwa.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Mvua na ngurumo za radi zinatarajiwa kwa baadhi ya maeneo.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Mvua na ngurumo za radi kwa baadhi ya maeneo zinatarajiwa.
Imetolewa na;
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA