Machapisho

MATARAJIO YA HALI YA HEWA KWA TAREHE 21 - 30 SEPTEMBA, 2023.

Pakua

MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 21- 30 SEPTEMBA, 2023

Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Mvua na ngurumo za radi zinatarajiwa katika maeneo machache.

Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla, hata hivyo maeneo machache yanatarajiwa kuwa na vipindi vifupi vya mvua nyepesi.

Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Mvua nyepesi katika maeneo machache zinatarajiwa.

Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Mvua na ngurumo za radi zinatarajiwa katika maeneo machache.

Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Vipindi vya ukavu vinatarajiwa.

Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Vipindi vya ukavu vinatarajiwa.

Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Vipindi vya ukavu vinatarajiwa.

Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Vipindi vya ukavu vinatarajiwa.

Imetolewa na:

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA