Machapisho

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI APRILI, 2023

Pakua

Dondoo za tathmini ya Machi, 2023 na mwelekeo wa Aprili, 2023:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Machi, 2023 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Aprili, 2023 nchini.

  • Katika kipindi cha wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Machi 2023, upungufu wa mvua ulijitokeza katika maeneo mengi nchini kutokana na uwepo wa kimbunga Freddy na kisha kufuatiwa na ongezeko la mvua katika wiki ya tatu na ya nne ya mwezi.
  • Katika mwezi Aprili 2023, vipindi vya mvua vinatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi sambamba na ongezeko la mvua katika baadhi ya maeneo.
  • Hali ya joto ya kawaida inatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo ya nchi kwa kipindi cha mwezi Aprili, 2023.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali pakua