Machapisho

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI FEBRUARI, 2023

Pakua

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Januari, 2023 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Februari, 2023 nchini.

  • Kipindi cha mwezi Januari 2023, maeneo mengi ya nchi yalipata mvua zilizosababishwa na uwepo wa Ukanda Mvua nchini pamoja na kimbunga ‘CHENESO’ kilichotokea katika eneo la kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar na kusababisha ongezeko la mvua katika baadhi ya maeneo nchini hususan katika wiki ya tatu ya mwezi Januari.
  • Katika mwezi Februari 2023, vipindi vya mvua vinatarajiwa kuendelea katika maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. Hata hivyo, mvua za nje ya msimu zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.
  • Vipindi vya joto vinatarajiwa kuendelea katika baadhi ya maeneo ya nchi hususan yale yanayotarajiwa kuwa na upungufu wa mvua.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali pakua