Machapisho
UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI NOVEMBA, 2022
PakuaDondoo za tathmini ya Oktoba, 2022 na mwelekeo wa Novemba, 2022:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Oktoba, 2022 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan mvua pamoja na hali ya joto kwa mwezi Novemba, 2022 nchini.
- Katika kipindi cha mwezi Oktoba, 2022 maeneo mengi ya nchi yaliendelea kuwa makavu. Hata hivyo, vipindi vichache vya mvua vilijitokeza katika maeneo machache ya ukanda wa pwani na ziwa Victoria.
- Katika mwezi Novemba, 2022 mvua za Msimu zinatarajiwa kuanza katika maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka hususan maeneo ya Magharibi mwa nchi. Hata hivyo, mvua zinatarajiwa kuendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka (pwani ya kaskazini, kanda ya Ziwa Viktoria na Nyanda za juu kaskazini mashariki).
- Kwa upande mwingine mvua za chini ya wastani sambamba na hali ya ongezeko la joto kiasi inatarajiwa katika baadhi ya maeneo nchini.