Machapisho
WELEKEO WA MSIMU WA MVUA ZA VULI (OKTOBA – DISEMBA, 2022) KWA MAENEO YA KASKAZINI MWA MKOA WA MOROGORO
PakuaDondoo • Kwa ujumla mvua za Chini ya Wastani hadi Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya mkoa wa Morogoro.
• Mvua zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya nne ya mwezi Oktoba na wiki ya kwanza ya Novemba, 2022. • Mvua zinatarajiwa kuisha Januari, 2023.
• Vipindi virefu vya ukavu vya siku kumi (10) au zaidi vinatarajiwa katika msimu huu wa Vuli.
Mvua za msimu wa Vuli, 2022 Kwa ujumla mvua zinatarajiwa kuwa za chini ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi ya wilaya za mkoa wa Morogoro. Msimu unatarajiwa kuanza kwa kusuasua na kuambatana na vipindi virefu vya ukavu. Angalizo: Ingawa maeneo mengi yanatarajiwa kupata mvua za chini ya wastani hadi wastani, izingatiwe kuwa matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa yanaweza yakajitokeza katika maeneo machache