Machapisho
Utabiri wa hali ya hewa wa mwezi Septemba, 2022
PakuaDondoo za tathmini ya Agosti, 2022 na mwelekeo wa Septemba, 2022:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Agosti, 2022 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto la chini pamoja na mvua kwa mwezi Septemba, 2022 nchini.
- Katika kipindi cha mwezi Agosti, 2022 maeneo mengi ya nchi yaliendelea kuwa makavu pamoja na vipindi vya baridi. Hali ya baridi zaidi ilijitokeza katika maeneo ya nyanda za juu Kusini magharibi na sehemu za miinuko za nyanda za juu Kaskazini mashariki.
- Katika mwezi Septemba, 2022 ongezeko kidogo la joto linatarajiwa katika maeneo mengi. Aidha, hali ya baridi inatarajiwa katika maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kusini magharibi na nyanda za juu kaskazini mashariki. Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache ya mwambao wa pwani, ukanda wa Ziwa Victoria na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki.