Machapisho

Utabiri wa hali ya hewa wa mwezi Agosti, 2022

Pakua

Dondoo za tathmini ya Julai, 2022 na mwelekeo wa Agosti, 2022:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Julai, 2022 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto la chini kwa mwezi Agosti, 2022 nchini.

  • Katika kipindi cha mwezi Julai, 2022 hali ya baridi iliendelea kujitokeza katika maeneo mengi ya nchi. Hali ya baridi zaidi ilijitokeza katika maeneo ya nyanda za juu Kusini magharibi na sehemu za miinuko za nyanda za juu Kaskazini mashariki.
  • Katika kipindi cha mwezi Julai, 2022 maeneo mengi ya nchi yaliendelea kuwa makavu. Aidha, vipindi vya mvua vilijitokeza katika maeneo machache ya mwambao wa pwani pamoja na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki. Kwa upande mwingine, vipindi vya upepo mkali vilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini yakiwemo maeneo ya ukanda wa pwani na maziwa makuu.
  • Katika mwezi Agosti, 2022 hali ya baridi inatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi ya nchi. Aidha, ongezeko kidogo la joto la chini linatarajiwa katika baadhi ya maeneo.
.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali pakua