Machapisho
Utabiri wa hali ya hewa wa mwezi Juni, 2022
PakuaDondoo za tathmini ya Mei, 2022 na mwelekeo wa Juni, 2022:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Mei, 2022 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto la chini kwa mwezi Juni, 2022 nchini.
- Katika kipindi cha mwezi Mei, mvua za Masika ambazo ni mahususi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua ziliendelea kunyesha katika maeneo machache. Hata hivyo, vipindi vichache vya mvua kubwa vilijitokeza katika maeneo machache ya pwani ya kaskazini.
- Katika mwezi Juni, 2022 hali ya joto la chini inatarajiwa kupungua hususan nyakati za usiku na asubuhi katika maeneo mengi ya nchi ikiashiria kuanza kwa msimu wa Kipupwe. Vipindi vya upepo mkali pia vinatarajiwa hususan katika maeneo ya ukanda wa pwani. Aidha, vipindi vichache vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache ya ukanda wa pwani na Ziwa Victoria.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali pakua