Habari
Imewekwa:
Aug, 08 2025
VIONGOZI WAKUMBUSHWA KUHAMASISHA WANANCHI KUTUMIA TAARIFA ZA TMA

Morogoro, tarehe 07 Agosti 2025
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bi. Pili Mnyema amewakumbusha viongozi mbalimbali nchini kuendelea na jitihada za kuhamasisha wananchi kutumia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari katika Maonesho ya Nane Nane 2025 yanayoendelea kwenye viwanja vya Nane Nane, Morogoro.
“Kama viongozi tunajukumu la kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi wetu ikiwemo wakulima, wafugaji na wavuvi ili watumie utabiri wa hali ya hewa unaotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, itawasaidia wananchi kudhibiti au kujikinga na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyopo”