Habari

Imewekwa: Oct, 17 2025

JAJI MSHIBE AWATAKA WASHINDI WA TUZO ZA HABARI ZA HALI YA HEWA 2025 KUTORUDI NYUMA

JAJI MSHIBE AWATAKA WASHINDI WA TUZO ZA HABARI ZA HALI YA HEWA 2025 KUTORUDI NYUMA

Dar es Salaam, tarehe 16 Oktoba 2025.

“Washindi wote mliopata tuzo za habari za hali ya hewa 2025 nawasihi msibweteke sababu nimeona washindi wengi waliopata TUZO mwaka jana hawapo mwaka huu, inapaswa ikiwa umepata tuzo mwaka huu basi mwaka unaofuata ufanye vizuri zaidi” Alizungumza hayo Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) na mgeni rasmi katika hafla ya utoaji TUZO za wanahabari bora wa habari za hali ya hewa kwa mwaka 2025 iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dar es Salaam, tarehe 16 Oktoba 2025.

Jaji Mshibe alianza kwa zoezi la kukabidhi Tuzo hizo za Wanahabari bora, ambapo mshindi upande wa Luninga na Redio alikuwa ni Lisungu Kambona kutoka ZCTV, mshindi upande wa Magazetini alikuwa ni Penina Malundo kutoka gazeti la Majira, mshindi kutoka Zanzibar tuzo ilichukuliwa na Amour Khamis Ali kutoka Assalam FM, mshindi upande wa Mitandao ya Kijamii alikuwa ni Juma Issihaka kutoka Mwananchi Digital

Jaji Mshibe aliongezea, kwa kuwataka waandishi wa habari kuendelea kutoa taarifa za hali ya hewa zenye uhakika na kwa weledi mkubwa huku akiwapongeza TMA kwa kuendelea na kuimarisha utoaji wa TUZO zinazoleta motisha kwa waandishi wa habari katika kuhabarisha na kuelimisha jamii kuhusu taarifa za hali ya hewa nchini.

Aidha, hafla hiyo ya tuzo ambayo n ya sita tangu kuanzishwa kwake mwaka 2019, ilitanguliwa na warsha ya wanahabari kuhusu mwelekeo wa mvua za msimu unaoanzia mwezi Novemba 2025 hadi Aprili 2026. Mamlaka inatarajia kutoa rasmi utabiri huo tarehe 17 Oktoba 2025, Ubungo Plaza