Taarifa za Hali ya Hewa Kilimo
Jarida la Hali ya Hewa Kilimo Lenye Tathmini ya Oktoba1-10, 2025 na Matazamio kwa Kipindi cha Oktoba 11-20, 2025
Pakua- Wakulima, hususan katika maeneo yanayopata mvua za Vuli wanashauriwa kupanda mazao mara tu udongo unapokuwa na unyevu nyevu wa kutosha kuotesha mbegu
- Wafugaji wanashauriwa kutumia malisho yaliyopo kwa uangalifu.
- Wadau wote wa kilimo wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa kwa mipango thabiti ya shughuli za kilimo.
TMA Jarida la Hali ya Hewa kilimo la Msimu wa mvua za VULI 2025
PakuaMvua zinatarajiwa kuwa za Wastani hadi Chini ya Wastani katika maeneo mengi na kutawaliwa na vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko wa
mvua usioridhisha hususan katika maeneo ya pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki.
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Oktoba, 2025 katika maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara na kaskazini
mwa mkoa wa Kigoma; na kusambaa katika maeneo ya pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki wiki ya kwanza na ya pili ya
mwezi Novemba 2025. Mvua zinatarajiwa kuisha mwezi Januari, 2026
Mvua za Vuli zinatarajiwa kuongezeka kidogo mwezi Desemba, 2025
Vipindi vya joto kali kuliko kawaida vinatarajiwa katika msimu huu wa Vuli.