Taarifa za Hali ya Hewa Kilimo
Jarida la Hali ya Hewa Kilimo lenye Tathmini ya Oktoba11-20, 2025 na Matazamio kwa Kipindi cha Oktoba 21-31, 2025
Pakua- Wakulima, hususan katika maeneo yanayopata mvua za Vuli wanashauriwa kupanda mazao mara tu udongo unapokuwa na unyevu nyevu wa kutosha kuotesha mbegu
- Wafugaji wanashauriwa kutumia malisho yaliyopo kwa uangalifu.
- Wadau wote wa kilimo wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa kwa mipango thabiti ya shughuli za kilimo
Jarida la hali ya Hewa Kilimo la msimu wa Novemba 2025 hadi Aprili_2026 (NDJFMA-Mvua za Msimu)
Pakua- Mvua za Chini ya Wastani hadi Wastani zinatarajiwa katika mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Singida na Dodoma na Wastani hadi Chini ya Wastani katika mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe, Rukwa, Ruvuma, Mtwara na Lindi pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro. Vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko wa mvua usioridhisha vinatarajiwa katika maeneo mengi.
- Mvua zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Oktoba, 2025 katika mikoa ya Tabora, Katavi na Kigoma; na kusambaa katika mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro kati ya wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Novemba, 2025 na kuisha kati ya wiki ya nne ya mwezi Aprili na wiki ya kwanza ya mwezi Mei 2026 katika maeneo mengi. Kipindi cha nusu ya pili ya msimu (Februari-Aprili, 2026) kinatarajiwa kuwa na ongezeko la mvua ikilinganishwa na nusu ya kwanza (Novemba, 2025-Januari, 2026).
- Mvua za Chini ya Wastani zinazotarajiwa katika maeneo mengi zinaweza zikasababisha upungufu wa unyevu wa udongo na kuathiri ukuaji na maendeleo ya mazao na kupunguza mavuno hususani kwa mazao yanayotegemea mvua.
