10 Days Forecast
MUHTASARI WA MWENENDO WA MVUA KWA TAREHE 21-31 MACHI, 2026 NA MATARAJIO YA MVUA KWA TAREHE 01-10 APRILI, 2026.
MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 01-10 APRILI, 2026.
Kanda ya ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa katika maeneo machache.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache.
Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Mvua zinatarajiwa katika maeneo machache.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Vipidindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache.
Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo.

