Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

ISO 9001:2015 Imethibitishwa Kutoa Huduma za Hali ya Hewa kwenye Usafiri wa Anga

Monthly Forecast

MUHTASARI WA HALI YA HEWA KWA MWEZI SEPTEMBA, 2026 NA MWELEKEO KWA MWEZI OKTOBA, 2026.

Dondoo za tathmini ya Septemba, 2026 na mwelekeo wa Oktoba, 2026:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Septemba, 2026 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto kwa mwezi Oktoba, 2026 nchini.

  1. Katika kipindi cha mwezi Septemba, 2026 maeneo mengi  nchini yaliendelea kupata vipindi vya baridi ya wastani, hususan nyakati za usiku na asubuhi.
  2. Vipindi vya upepo mkali vilijitokeza katika baadhi ya maeneo katika kipindi cha mwezi Septemba 2026, hususan ukanda wa pwani, kanda ya kati pamoja na maziwa makuu. Aidha, vipindi vya mvua vilijitokeza katika maeneo machache ya mwambao wa pwani, ukanda wa ziwa Victoria na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki pamoja na nyanda za juu kusini magharibi.
  3. Katika kipindi cha mwezi Oktoba 2026, mvua za Vuli zinatarajiwa kuanza katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Aidha, mvua za Juu ya wastani hadi wastani zinatarajiwa katika maeneo hayo.

Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua