Habari,
Ninayo furaha na heshima kubwa kwa niaba ya menejimenti na wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kukukaribisha katika tovuti hii mahususi na rasmi ya TMA.
Katika tovuti hii utapata taarifa muhimu kuhusu TMA ikiwemo Dira, kazi na majukumu yake , kama yalivyo ainishwa katika sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa namba 2 ya mwaka 2019.
Tovuti hii imefanyiwa maboresho ili kuimarisha na kuboresha huduma za TMA kwa wananchi na wadau. Maboresho yaliyofanyika yanawezesha upa...
Habari,
Ninayo furaha na heshima kubwa kwa niaba ya menejimenti na wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kukukaribisha katika tovuti hii mahususi na rasmi ya TMA.
Katika tovuti hii utapata taarifa muhimu kuhusu TMA ikiwemo Dira, kazi na majukumu yake , kama yalivyo ainishwa katika sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa namba 2 ya mwaka 2019.
Tovuti hii imefanyiwa maboresho ili kuimarisha na kuboresha huduma za TMA kwa wananchi na wadau. Maboresho yaliyofanyika yanawezesha upatakanaji wa taaarifa uwe rahisi na kwa njia rafiki zaidi. Tovuti inawezesha upatikanaji kwa urahisi taarifa za tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa, utabiri wa saa ishirini na nne, siku tano, siku kumi na utabiri wa Msimu. Utabiri wa siku kumi na wa mwezi mahususi kwa shughuli za kilimo pia unapatikana kwa urahisi.
Tovuti inatoa fursa ya kupata video na picha za matukio mbalimbali ya hali ya hewa.
Tovuti hii imeunganishwa pia na mifumo kadhaa inayotumika katika shughuli za Mamlaka, aidha tuvuti hii imeunganishwa na baadhi ya tovuti mashuhuri ili kukurahisisha upatikanaji wa taarifa.
Mamlaka itaendelea kuboresha Tovuti hii kila itakapobidi ili kuhakikisha wewe mwananchi na mdau unapata taarifa kwa wakati.
Asante sana kwa kutembelea Tovuti yetu.
Dkt. Ladislaus Chang'a
Kaimu Mkurugenzi Mkuu