Mkurugenzi Mkuu
Dkt.Ladislaus Chang'a
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
WasifuWasifu
Dk. Ladislaus Benedict Chang'a ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) tangu Novemba 2022. Pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (Intergovernmental Panel on Climate Change-IPCC). Dk. Chang’a ni mwanasayansi mbobevu katika sayansi ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi mwenye uzoefu mkubwa katika fani hii. Ana uzoefu katika uangazi na ufuatiliaji wa hali ya hewa; uchakataji na uchambuzi wa data za hali ya hewa; utabiri wa hali ya hewa; mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi. Ameshiriki katika kuongoza na kusimamia majadiliano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi katika mikutano ya Umoja wa Mataifa (UNFCCC). Amefanya kazi katika nafasi ya Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa katika TMA kuanzaia mwaka 2014, na pia amekuwa akifundisha masomo ya Sayansi ya Hali ya Hewa kwa muda wa ziada katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Ardhi, na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ambapo amefundisha kozi za uangazi na ufuatiliaji wa Hali ya Hewa na utabiri wa hali ya hewa na sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi pamoja na kuwasimamia wanafunzi katika kazi zao za utafiti
Mkurugenzi Mkuu
